
Msanii
wa Hip Hop nchini Tanzania, aliyekuwa chini ya Ostaz Juma, Janjaro kutoka Mjini
Arusha, kwasasa anaishi JIJINI DSM, amefunguka na kusema kuwa amejitoa kwa
Ostaz kwa mapenzi yake mwenyewe wala hakufukuzwa na Ostaz.
Aliendelea
kwa kusema kuwa amechoshwa na mambo ya Ostaz kwa muda mrefu sasa pia anataka
kuwa msanii huru na kufanya kazi zake mwenyewe kama wasanii wengine
wanavyofanya.
“
najua yatasemwa mengi kutoka kwa Ostaz juma ila mimi ndio uwamuzi wangu, kuna
watu wanasema sina nidhamu lakini lakini hao watakuwa wanajijua sasa hivi
hawakunifuatilia kutoka nyuma. Hata mtoto mdogo atakuwa mtundu ila akiwa mkubwa
hunyooka na kuwa mtoto mzuri sasa nimekuwa mkubwa na kupelekwa pelekwa tena
sitaki. Hayo yalikuwa maneno ya Janjaro mara alipokuwa anafanyiwa mahojiano na
Dj Choka.
0 maoni:
Post a Comment