Mkuu wa Umoja wa Mataifa
anayeshughulika na msaada wa dharura, , Valerie Amos, ametoa wito mapigano
yasitishwe katika kitongoji cha mji mkuu wa Syria, Damascus, ili kuruhusu
chakula na madawa kupelekwa.
Alisema
ingawa watu maelfu walikihama kitongoje cha Moadamiyet, juma lilopita, hata
hivo maelfu bado wamenasa.
Matamshi
yake yanafanana na yale ya wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Marekani,
ambayo iliitaka Syria iruhusu msaada wa dharura ufikishwe vitongoji - vitongoji
vinavyodhibitiwa na wapiganaji na ambavyo vimezingirwa na jeshi la serikali.
Katika
tukio jengine, wanaharakati wanasema kuwa wanajeshi kama 16 wameuwawa kwenye
mripuko wa bomu lilotegwa kwenye gari katika kitongoji cha Jaramana, ambacho ni
kitiifu kwa Rais Assad.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment