Watu watatu akiwemo msichana mdogo mwenye umri wa miaka 8 aliuawa wakati
watu waliokuwa wamejihami wakiwa kwenye pikipiki kushambulia sherehe za ndoa
nje ya kanisa la Kikopti mjini Cairo.
Takriban wengine 9 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo mjini
Giza.
Hata hivyo hakuna taarifa zozote kuhusu nani aliyehusika na
shambulizi hilo.
Jamii ya wakristo wa kikopti wamekuwa wakishambuliwa na baadhi
ya waisilamu wanaotuhumu kanisa kwa kuunga mkono jeshi katika kumpindua
aliyekuwa Rais Mohammed Morsi mwezi Julai.
Washambuliaji hao ambao hawakutambuliwa, waliwafyatulia risasi
kiholela watu waliokuwa wanaondoka kanisani.
Mwanamume mmoja na mtoto huyo waliuawa nje ya kanisa hilo wakati
mwanamke mmoja akifariki akipelekwa hospitalini.
"Tulisikia mlio mkubwa sana mfano wa kitu kilichokuwa
kinaanguka,’’ alisema shahidi mmoja.
"Nilimkuta mwanamke mmoja akiwa ameketi kwenye kiti chake,
akiwa amejeruhiwa kwa risasi. Watu wengi walikuwa wameanguka kando yake akiwemo
mtoto mdogo.’’
Kasisi wa kanisa hilo Thomas Daoud Ibrahim alisema kuwa alikuwa
ndani ya kanisa hilo, wakati, milio ya risasi ilikuwa inasikika.’’
"Kilichofanyika ni kitu kibaya sana na sio waksristio
wakopti waliolengwa pekee yao , tunaharibu nchi yetu,’’ alisema kasisi huyo.
Kasisi mwingine aliambia vyombo vya habari kuwa kanisa hilo
liliachwa bila polisi wala mlinzi tangu mwishoni mwa mwezi Juni.
Kanisa hilo ni moja ya makaisa ya zamani ya kikristo
iliyoanzishwa mjini
Alexandria mapema miaka ya 50 AD.
Idadi ya wakristo nchini Misri ni asilimia 10 ikiwa waumini
milioni 80, na wamekuwa wakiishi kwa amani na waisilamu wa kisunni kwa miaka
mingi.
Hata hivyo, kuondolewa mamlakani kwa Morsi kijeshi, kumefuatiwa
na mashambulizi mabaya dhidi ya makanisa na rasilimali za waumini hao kwa miaka
mingi.
Wakati mkuu wa majeshi Generali, Abdul Fattah al-Sisi,
alitangaza kwenye televisheni kuwa rais Morsi aliondolewa mamlakani baada ya
maandamano makubwa yakimtaka ajiuzulu aliandamana na papa Tewadros.
Tewadros alisema kuwa mkakati uliofikiwa na Al-asisi ulitokana
na mawazo ya viongozi waheshimiwa ingawa hakuwataja.
Kutoka
BBC
0 maoni:
Post a Comment