Kweli mwisho wa mwaka uwa na vitimbwi vya kila namna, sasa leo hii ilitokea kali ya jama mmoja asiyefahamika, kupanda katika mnara wa Vodacom, uliopo mkabala na Ofisi za TBS, uku akiwa na Document na baadhi ya picha, alipotakiwa kushuka chini alijibu kuwa hashuki mpaka Rais Kikwete afike eneo la tukio.
Yasemekana kuwa huyo jamaa alishawai kufungwa bila
kosa kwa muda wa miaka 6, hivyo aliitaji akutane na Kikwete ili aweze
kumfikishia lawama zake.
Kikosi cha zima moto na uokoaji waliweza kumshusha na
kumfikisha katika kituo cha Polisi.
0 maoni:
Post a Comment