Mrembo wa Kenya Lupita Nyong’o ambaye ameigiza kama
star kwenye filamu ya Hollywood ‘12 Years a Slave’ iliyomkutanisha na waigizaji
maarufu akiwemo Brad Pitt, hakuonekana kwenye uzinduzi wa filamu hiyo jana
(December 27).
Kutohudhuria kwake kwenye uzinduzi wa filamu hiyo
kumeunganishwa na suala la ubaguzi wa rangi uliojitokeza katika posters za
filamu hiyo ambazo zinawaonesha waigizaji ‘wazungu’ na kumuweka pembeni Lupita
Nyong’o ambaye amechukua nafasi kubwa katika filamu hiyo.
Hata hivyo msemaji wa kampuni ya Lionsgate wanaohusika
na uuzaji wa filamu hiyo, amesema kuwa kutoonekana kwa Nyong’o katika uzinduzi
huo hakuna uhusiano na utata uliojitokeza katika posters za filamu hiyo.
Amesema kuwa muwakilishi wa Nyong’o aliwaambia
waandaaji wa tukio hilo
wiki mbili kabla kuwa muigizaji huyo asingehudhuria.
Posters zilizotolewa zimeonesha ubaguzi baada ya
kuwaweka pembeni waigizaji wengine ambao wamechukua nafasi kubwa katika filamu
hiyo kama Lupita Nyong’o na Chiwetel Ejiofor,
na badala yake wameonekana Brad Pitt na Michael Fassbender.
Hata hivyo Summit Entertainment waliomba radhi kwa
posters hizo na kudai kuwa hazikuwa zimeruhusiwa na uongozi, na hivyo kupiga
marufuku usambazaji wa posters hizo.
Kutoka timesfm
0 maoni:
Post a Comment