Baada ya member wa zamani wa kundi la G-Unit, Mazaradi
Fox kuuawa kwa kupigwa risasi ijumaa ya wiki iliyopita polisi wameeleza kuwa
kifo chake kimetokana na kulipizana visasi kwa makundi ya kihalifu.
Kwa mujibu wa New York Daily News, maafisa wa polisi
wameeleza kuwa miaka mitano iliyopita marehemu Mazaradi Fox aliwahi kumfyatulia
risasi Rashawn Carter ambaye ni member kundi moja la kihalifu katika eneo ya
Queens. Lakini mtu huyo aliweza kunusurika japo alipata majeraha.
Wamesema kufuatia tukio hilo Fox alitupwa jela baada
ya kukutwa na hatia ya kufanya jaribio la kuua, na baadae kuachiwa huru
alipomaliza muda alioamriwa kukaa jela.
Nalo kundi la G-Unit lilitoa tamko January 3 na
kuonesha kushitushwa na taarifa za Fox. Muwakilishi wa kundi hilo pamoja na kutoa
pole kwa familia ya marehemu, alisema 50 Cent alipata taarifa hizo akiwa katika
studio zake New York na kwamba alishitushwa sana na habari hizo.
0 maoni:
Post a Comment