Mez B anusurika kifo baada ya kushambuliwa vibaya na kisu na mtu asiyemfahamu. Msikilize hapa akisimulia
Member wa kundi la Chember Squad Mez B wa Area C Dodoma, amenusurika kifo baada ya kushambuliwa vibaya na mtu asiyemfamu, Ijumaa (January, 2014).
Mkali huyo ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa alikuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa sita usiku alipokuwa akitoka kwa member mwenzake wa Chember Squad Noorah, na kwamba akiwa njiani alikutana na mtu asiyemfahamu ambaye alikuwa anatoa matusi mengi kwa Rais kitendo kilichomfanya amshauri kiungwana kuacha anachokifanya.
“Yaani hakuna tatizo lolote kubwa, kwa sababu yeye ndiye alikuwa anatukana. Mara anamtukana Rais mara nini…mpaka sasa ikabidi friendly tu nimuulize, nikamwambia ndugu yangu basi bora ututane sisi sasa unamtukana hadi rais wa nchi yako? Au we foreigner sio raia nini? Unaona eeh jamaa anaonekana kama mtu wa Rwanda au Burundi.” Mez B ameiambia tovuti ya Times Fm.
“Basi ikawa hivyo mimi nilivyomuuliza ndo ikawa hivyo nilivyomuuliza ikaisha pale, then baada ya hapo ndo ikatokea matatizo hayo muda kama wa saa sita usiku…kwanza nilienda polisi nikakata PF3 halafu ndo nikaenda hospitali. Noorah nilimpa taarifa baadae kwa sababu hata simu sikujua ilikuwa wapi kwa sababu nilianza kutoa taarifa kesho yake kwa sababu nililazwa pale mpaka kesho yake jioni.” Mez B amesimulia.
Amesema mtu huyo alimshambulia vibaya na kisu usoni na kumjeruhi, na kwamba walinzi na mabaunsa waliokuwepo walikuwa wanamuangalia tu kama vile walipanga. Lakini kwa sasa anaendelea vizuri.
Msikilize hapa akisimulia kiundani.
KUTOKA timesfm.
0 maoni:
Post a Comment