Mchezaji wa Manchester City ambaye pia hucheza nafasi ya kiungo cha
kati katika timu ya Ivory Coast, Yaya Toure ndiye mwanasoka bora zaidi mwaka
2013 barani Afrika
Toure alikabidhiwa tuzo la (caf) mwaka wa tatu mfululizo katika sherehe
zilizofanyika mjini Lagos, Nigeria Alhamisi usiku.
Aidha Toure pia alishinda tuzo la BBC la mwanasoka bora zaidi barani
Afrika mwaka jana.
Alikuwa anawania tuzo hilo dhidi ya mchezaji mwenzake wa Ivory Coast
Didier Drogba, ambaye huchezea Galatasaray na John Mikel Obi mnigeria ambaye
husakata soka nchini Uingereza.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment