
Msanii wa hip hop , Tanzania, kutoka Tongwe Records,
Roma Mkatoliki, amefunguka na kusema kuwa yuko mbioni kuachia ngoma yake mpya
wiki ijayo, jina la ngoma hiyo ni “KKK” ikiwa ni katika Project yake mpya ya “
The Return of The Ninja”...........
“Tunaplan kuitoa siku yoyote kuanzia wiki ijayo yaani
kuanzia jumatatu. Inaweza kuwa Jumatatu hiyo hiyo ama jumanne, ama jumatano.
Kwa nini hatuko sure…kwa sababu Tongwe kuna wasanii wengi ambao wanatakiwa
kutoka pia...ndo maana hatuko sure na tarehe lakini tuko sure na wiki. Wimbo
utatoka wiki ijayo, unaitwa ‘KKK’ yaani triple K, umefanyika Tongwe records kwa
producer J-Ryder pamoja
usimamizi mzima wa C.E.O wetu wa Tongwe ambaye ni J-Marder.” Alifunguka Roma.
“Kwa takribani miaka sita ama saba nilikuwa na system hiyo ya kutoa wimbo mmoja kwa mwaka toka 2007 tunaanza na wimbo wa kwanza. Lakini time inaenda na vitu vingi vinaenda vinabadilika. Kwa hiyo kitu ambacho Roma anakuja nacho 2014 hatatoa wimbo mmoja kama ilivyozoeleka, nina plan ya kutoa nyimbo kama tatu kwa sababu nyimbo zinarekodiwa kila siku. Kwa hiyo wimbo wa kwanza tunautoa mwanzo wa mwaka, katikati ya mwaka kwenye June hivi naweza kutoa wimbo mwingine na mwishoni mwa mwaka naweza kutoa wimbo mwingine.” Hayo yalikuwa maneno ya Roma.
0 maoni:
Post a Comment