
Wastani wa mshahara nchini Burkina faso ni
takriban dola 150 kwa mwezi, kwa mujibu wa Mbunge kutoka baraza la mpito nchini
humo ,mishahara inahusisha malipo ya vikao vya bunge, malipo ya shughuli za
ofisi, malipo kwa ajili ya huduma za afya na gharama za mafuta...............
Lakini
Mratibu kutoka asasi moja ya kiraia ya nchini humo Herve Kam anasema malipo ya
baada ya kuhudhuria bunge hayakupaswa kuwapo akieleza kuwepo kwa utofauti
mkubwa kati ya Maafisa wa serikali na raia wa kawaida.
Tangu
mwezi Oktoba mwaka jana Rais Blaise Compaore alipoondolewa madarakani, baraza
la mpito lilikuwa na wawakilishi 90 ambao waliwakilisha lililokuwa bunge la
nchi hiyo.
Mmoja
wa wabunge anaunga mkono hatua hii ya kupunguza mishahara akisema hatua hii
inaimarisha utawala bora na demokrasia thabiti.
Hali
ilikua ya mtafaruku Baada ya kubainika kwa kiasi cha mishahara ya wabunge hali
iliyosababisha ghadhabu miongoni mwa jamii kupitia kwenye mitandao wakikemea
kile walichodai kutotendewa haki na kutaka viongozi kuacha kutumia madaraka yao
vibaya.
Baada
ya kupambana kubadilisha Serikali ya Burkinafaso, raia nchini humo wana
matumaini ya kuweka mfumo mpya na mzuri wa haki.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment