Kamanda mkuu wa kundi la waasi la LRA
nchini Uganda Dominic Ongwen amewasili mjini Hague ambako atafunguliwa
mashitaka ya uhalifu wa kivita..............
Ongwen,
alikuwa kamanda mwenye kuogopewa sana katika kundi la waasi la LRA na
alikamatwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati mapema mwezi huu.
Uganda
ilikubali kwamba muasi huyo apelekwe katika mahakama ya kimataifa ya
ICC, licha
ya nchi hio kuwa mkosoaji mkubwa wa mahakama hio.
Wanajeshi
wa Marekani wakishirikiana na wa Afrika, wamekuwa wakifanya msako
dhidi ya
Ongwen tangu mwaka 2011.
Anasemekana
kua naibu wa kiongozi wa LRA Joseph Kony ambaye bado yupo mbioni.
ICC
ilisema kwamba Ongwen atazuiliwa katika kituo kimoja nchini Uholanzi hadi
mahakama itakapokuwa tayari kusikiliza kesi yake.
Alitarajiwa
kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu alipowasili Hague huku tarehe ya kusikilizwa
kwa kesi yake ikisubiriwa.
Taarifa
ilitolewa na Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na katibu mkuu wa
umoja huo ikipongeza hatua ya kumpeleka Ongwen mjini Hague.
Ban
alisema ni hatua kubwa katika kuhakikisha kwamba waaathiriwa wa unyama
uliotendwa na LRA wanapata haki.
Kiongozi
wa kundi la waasi la LRA nchini Uganda ambaye anatakikana na ICC
'Matumaini
kwa waathiriwa'
Msemaji
wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Jen Psaki pia amepongeza hatua ya
kukamatwa kwa muasi huyo akisema inatoa matumaini makubwa kwa waathiriwa wa
uasi wa kundi la LRA.
Tunawataka
waasi wengine wa kundi la LRA waliosalia kufuata nyayo za Ongwen na wapiganaji
wengine wa kundi hilo waliojisalimisha tangu mwaka 2012, kusalimisha silaha zao
na kurejea nyumbani.
Marekani
sio mwanachama wa mkataba wa Roma uliosaidia kuundwa kwa mahakama ya ICC lakini
licha ya hilo, ilisaidia katika kumkabidhi muasi huyo kwa ICC.
Awali
ilitoa ahadi ya zawadi ya dola milioni 5 kwa yeyote ambaye angetoa taarifa
kumhusu Ongwen na kupelekea kukamatwa kwake.
Anatuhumiwa
kwa madai ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu ikiwemo kutumia
waathiriwa kama watumwa.
Uasi
wa LRA ulianza zaidi ya miaka 20 iliyopita kaskazini mwa Uganda na inakisiwa
kati ya wpaiganaji 200-500 wameteswa na waasi wa kundi hilo nchini DRC, katika
Jamuhuri ya Afrika ya Kati,
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment