
Nigeria haihitaji msaada wa Vikosi vya
Umoja wa Mataifa kupambana na Boko Haram.Mshauri wa maswala ya usalama wa taifa
nchini humo ameiambia BBC................
Sambo
Dasuki amesema Nigeria na majirani zake Niger,Chad na Cameroon wanamudu
kusshughulikia swala la Wanamgambo wa kiislamu.
Dasuki
amekiri kuwa Wanamgambo ni tishio kubwa la usalama nchini humo na kusema kuwa
takriban asilimia 50 ya Jeshi la Nigeria limepelekwa kaskazini mashariki .
Amesema
hatua hiyo inaashiria namna Jeshi lilivyolichukulia swala hili kwa umakini
mkubwa.
Alipoulizwa
na Kipindi cha Newsday cha BBC kama Nigeria inahitaji msaada wowote wa nje ,
alisema ''hapana''
Wanamgambo
wa Boko Haram walianza Operesheni yao mwaka 2009, wakidai kuwa wanataka kuunda
taifa la kiislamu.
Tangu
Serikali ilipotangaza hali ya hatari miezi 20 iliyopita kaskazini mashariki ili
kupambana na Wanamgambo, kundi hilo limejiimarisha na sasa linadhibiti miji
kadhaa .
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment