Waziri wa usalama nchini Kenya Joseph
Nkaissery amewaomba radhi wanafunzi wa shule ya msingi waliofyatuliwa gesi ya
kutoa machozi wakati walipokuwa wakiandamana kupinga unyakuzi wa kipande cha
ardhi ambacho kilikuwa uwanja wao wa kuchezea.............................
Bwana
Nkaissery amempa mnyakuzi wa ardhi hio siku moja kuondoa sehemu ya ukuta
iliobaki baada ya wanafunzi kuuangusha na kisha kuondoka katika eneo hilo.
Nkaisery
ameongeza kwamba serikali itaweka uzio katika ardhi hio na kuiwacha kuwa
uwanja
wa kuchezea wa wanafunzi hao.
Wakati
huohuo, amewaonya wanaharakati dhidi ya kukiuka sheria kila wakati
wanapojiandaa kufanya maandamano badala ya kuchukua sheria mikononi mwao.
Wanafunzi
waliofyatuliwa gesi ya kutoa machozi kwa kuandamana kupinga unyakuzi wa uwanja
wao
Mnamo
Jumatatu, wanafunzi watano na polisi mmoja walijeruhiwa katika vurugzu
zilizotokea baada ya wanafunzi kuandamana kupinga unyakuzi wa ardhi yao kutoka
kwa mtu aliyekuwa na mipango ya kufanya ujenzi.
Wakenya
wamekosoa polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya wanafunzi , hali
ambayo imesababisha afisa ammoja mkuu kusimamishwa kazi kwa mda.
Shirika
la kutetea masilahi ya watoto, la Save The Children, pia limelaani kitendo cha
polisi dhidi ya wanafunzi hao ambao walikuwa wanaandamana kwa amani kutetea
uwanja wao uliokuwa umenyakuliwa.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment