Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa
Marekani John Kerry, anapanga kukutana leo na Waziri mwenzake wa Urusi Sergey
Viktorovich Lavrov, kando na mkutano unaoendelea wa umoja wa mataifa huko mjini...................
Geneva
kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo.
Huu
ndio utakuwa mkutano wao wa kwanza tangu Kerry amzome Lavrov kwa kudanganya
kuhusu mchango wa Urusi katika mapigano yanayoendelea nchini Ukraine.
Mkutano
huo vilevile unasadifiana na kutolewa kwa ripoti maalum ya Umoja wa mataifa
inayoshtumu vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu mashariki mwa Ukraine.
UN
inasema kuwa zaidi ya watu 6000 wameuawa tangu mapigano hayo yaanze huku mamia
wakiuawa katika majuma machache yaliyopita.
Bwana
Kerry anatarajia kuzua mjadala kuhusiana na mauaji ya kiongozi wa upinzani
ambaye pia ni mpinzani sugu wa rais Putin Boris Nemtsov
Kiongozi
huyo alipigwa risasi na kuuawa karibu na makao makuu ya urais wa urusi Kremlin
siku ya ijumaa iliyopita.
Huku
hayo yakijiri, Tume ya jumuia ya Bara Ulaya inatazamia kufanya mazungumzo kati
ya Moscow na Kiev, ili kutazua tatizo lililoko kuhusiana na usambazaji wa gesi.
Juma
lililopita kampuni kubwa ya uuzaji gesi, Gazprom, liliwaonya wasambazaji wake
kuwa itakomesha pakubwa uuzaji wake wa gesi nchini Ukraine hadi Ukraine kutuma
malipo yake ya gesi mwezi huu wa Machi.
Aidha
mataifa hayo mawili yanatofautiana kuhusiana na usambazaji wa awali wa gesi kwa
makundi ya wapiganaji mashariki mwa Ukraine.
Mwezi
uliopita, Kiev ilisimamisha kutuma gesi hadi katika maeneo yaliyojitenga,
ikidai kuwa mabomba ya kupitishia mafuta na gesi yameharibiwa huku kampuni ya
Gazprom ikiwasambazia waasi mafuta moja kwa moja.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment