Karibu watu 70 wamefariki huko mashariki
mwa Nigeria baada ya lori la kubeba mafuta kushika moto...............
Police
wanasema huenda kilichosababisha moto huo ni ajali.
Walioshuhudia
wanasema dereva wa gari hilo alishindwa kulidhibiti ndiposa likakosa mwelekeo
na kutoka barabarani na kuwagonga watu waliokuwa wakisubiri usafiri katika
kituo kimoja cha mabasi.
Mmoja
ya waliokuwa wakishughulika kuwanusuru waliojeruhiwa amesema magari mengine 12
nayo yalishika moto.
Mwandishi
wa BBC aliyeko Nigeria anasema mikasa ya ajali zinazohusu magari ya kubeba
mafuta hutokea mara kwa mara nchini humo.
Miaka
mitatu iliyopita ajali mbaya sana ya moto wa mafuta iliwaua zaidi ya watu 100
huko Niger Delta katika mkasa uliochangiwa na watu kuchota mafuta yaliomwagika
baada ya gari kubwa la mafuta kupata ajali.
0 maoni:
Post a Comment