Serikali nchini Mexico
imetangaza kiangaza macho cha dola milioni 4 kwa yeyote ambaye atasaidia
kukamatwa kwa mfanyibiashara mkubwa zaidi wa madawa ya kulevya ambaye alitoroka
kutoka jela lenye ulinzi mkali huko Mexico.........
Shughuli kubwa ya
kumtafuta Joaquin Guzman ambaye pia anajulikana kama ''Shorty'' alitoroka
gerezani akipitia njia ya chini kwa chini .
Wakati wa mkutano na
waandishi wa habari waziri wa masuala ya ndani alisema kuwa maafisa katika
gezera hilo ni lazima walimsaidia Guzman kutoroka.
Aliongezea kusema kuwa
endapo itathibitishwa kuwa ukweli alisaidiwa na maafisa wa idara ya Magereza
basi hicho kitakuwa ni kitendo cha uhaini.
Maafisa watatu wa vyeo
vya juu wa gereza hilo akiwemo mkurugenzi wa gereza wamefutwa kazi.
Waziri wa mambo ya
ndani wa Mexico ameitisha mkutano wa magavana wa majimbo ili kujadili namna ya
kuepusha vurugu zinazoweza kutokea kufuatia kutoroka kwa mtuhumiwa maarufu wa
biashara ya dawa za kulevya.
Vyombo vya usalama
ndani ya Mexico na maeneo ya jirani kwa sasa vina msaka Joaquin Guzman
anayedaiwa kuwa ni mfanyabiashara nguli wa dawa za kulevya anadaiwa kutoroka
katika mazingira yanayodaiwa kuwa ni ya rushwa.
Naye Rais wa Mexco,
Enrique Pena Nieto, anasema kuwa ana Imani kuwa idara za usalama zitamkamata
mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuwa mhimili duniani kwa biashara hiyo ya dawa za
kulevya na ambaye alitoroka kutoka kati kati ya ulinzi mkali.
Hata hivyo Rais Pena
Nieto amesisitiza kuwa uchunguzi wa kina unatakiwa kufanywa kubaini aliko
Joaquin Guzman.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment