Shirika moja la kujtetea haki limeihsutumu
mojawepo ya kampuni kubwa zaidi duniani ya mauzo ya mawese, iliyoko nchini
Liberia, kwa kutumia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kujitajirisha............
Shirika
hilo, Global Witness, limesema kuwa wakati mlipuko huo ulipokuwa kilele Afrika
Magharibi mwaka uliopita, kampuni ya Golden Veroleum ilifyeka maelfu ya ekari
kwa maandalizi ya upanzi wa mmea huo wakati ambapo makundi ya missada kwa jamii
yalikuwa yanashughulika na kuokoa maisha ya watu kutokana na ugonjwa huo.
Hata
hivyo kampuni hiyo imejibu katika barua walioandika kwa shirika hilo la Global
Witness kuwa kandarasi ya pekee waliosaini mwaka huo, ilitokana na kazi zao za
miezi au hata miaka kabla ya kuzuka ugonjwa huo.
Wanaharakati
wa mazingira wamekuwa wakilaumu wakulima wa mashamba makubwa ya mawese kwa
uharibifu wa mazinginra na ongezeko la joto duniani
Chanzo BBC Swahili.
0 maoni:
Post a Comment