Kampuni kubwa zaidi duniani za mitandao ya
kijamii Google,Facebook na Twitter zimekubaliana kuondoa utupu katika mitandao
yao............
Hii
inafuatia kuenea kwa picha za utupu za watoto kwenye mitandao ya kijamii.
Mashirika
hayo kwa ushirikiano na shirika la kijamii linalopigania haki za watoto 'Internet
Watch Foundation' (IWF) sasa yameanza kuorodhesha picha za utupu wa watoto kwa
nia ya kuziondoa
Wakitumia
mbinu mpya ya kufichua watu wanaoshiriki ngono na watoto , IWF
inakusudia
kukomesha kudhalilishwa kwa watoto.
Hata
hivyo mbinu hiyo imekosolewa na wadau wa maswala ya mtandao wa intanet ambao
wanasema kuwa bado kuna mbinu fiche ya kusambaza picha hizo nje ya mitandao
hiyo kubwa ya kijamii.
Mwaka
uliopita waziri mkuu wa Uingereza David Cameron alionya kuwa shirika la
kijasusi nchini humo litaanza ushirikiano na mashirika ya kijamii kukabiliana
na kuenea kwa maeneo fiche kwenye mitandao ya intanet kwa nia ya kuwakamata
watu wanaowadhalilisha watoto kingono
Chanzo BBC Swahili.
0 maoni:
Post a Comment