Sherehe za ufunguzi wa ubalozi wa Marekani
huko Cuba zimefanyika mjini Havana..................
Hii
ndio mara ya kwanza kwa ubalozi huo na haswa bendera ya Marekani kupepea tena
nchini humo tangu mwaka wa 1961.
Waziri
wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, aliyeko Havana ndiye aliyekuwa mgeni
mheshimiwa katika dhifa hiyo ya kufungua upya ubalozi wa nchi yake nchini Cuba baada
ya zaidi ya nusu karne ilipofungwa.
Katika
sherehe zilizofanyika Havana, Kerry aliandamana na wanajeshi watatu wa zamani
ambao waliishusha bendera ya Marekani katika jengo la ubalozi huo mnamo 1961.
Rais
Obama na mwenzake wa Cuba Raul Castro walikubaliana mnamo December mwaka jana
kuurudisha uhusiano wa kidiplomasia.
Marekani
imelegeza baadhi ya vikwazo vya biashara na usafiri, hatahivyo bado vingine
vingi vingalipo.
kutoka BBC Swahili.
0 maoni:
Post a Comment