Rick Ross yupo matatani
kupelekwa tena mahakamani Kufuatia tuhuma za ubakaji wa Msichana mmoja huko Los
Angeles.
Kwa mujibu wa mtandao
wa TMZ Marekani, Rick Ross na rafiki yake Thaddeus “Black” James wanashtakiwa
na mwanamke asiejulikana jina kwa ubakaji… mwanamke huyo anadai kuwa alialikwa
na rapper huyo pamoja na rafiki yake kwenye party Los Angeles iliyokuwa inafanyika kwenye
hoteli moja yenye jina W Hotel.
Kutokana na maelezo ya
mtandao wa TMZ, Rick Ross na mwenzake walimfuata mwanamke huyo na gari kuelekea
kwenye party hiyo… alivyokuwa kwenye gari hilo Rick Ross akamualika glasi ya
kinywaji, alipojaribu kukataa baadhi ya marafiki zake Rick waliokuwa kwenye
gari hilo walimlazimisha kunywa kinywaji hicho.
Baada ya kunywa glasi
hiyo mwanamke huyo hakukaa muda akapoteza fahamu, alipozinduka akapewa glasi
nyingine ya kinywaji, hakukaa sana akapoteza fahamu tena kwa mara ya pili,
alipoaamka kesho yake aliona michubuko sehemu zake za siri zikiashiria mtu
alimwingilia kwa nguvu!
0 maoni:
Post a Comment