Mamia ya wafungwa
katika Gereza moja nchini jamuhuri ya Afrika ya kati wametoroka wakati ambapo
kumekuwa na machafuko yaliyosababisha watu kupoteza maisha.
Baada ya Dereva wa Taxi
muumini wa dini ya kiislamu kuuawa, mapigano yalizuka siku ya jumamosi kati ya
wanamgambo wa kikristo na makundi ya kiislamu.
Wafuasi wa wanamgambo
wa kikristo wajulikanao kwa jina anti-balaka walishambulia gereza siku ya
jumatatu, na kuwatorosha mamia ya Wanajeshi na wanamgambo.
Jamuhuri ya Afrika ya
kati imekuwa ikikumbwa na machafuko tangu kundi la waasi wa kiislamu, Seleka
kuchukua madaraka mwezi Machi mwaka 2013.
Kundi la Seleka baadae
liliondolewa madarakani, hali iliyosababisha machafuko.Maelfu ya watu
waliyakimbia makazi yao.
Tangu machafuko mapya
kuanza wikiendi, zaidi ya watu 30 wameuawa.
Shirika la kuhudumia
watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF limesema watoto watatu waliuawa na mmoja kwa
kuchinjwa.
Shirika la habari la AP
limesema Watu 500 wametoroka gereza la Ngaragba lililopo mji mkuu wa nchi hiyo,
Bangui siku ya jumatatu jioni.
Rais wa mpito wa nchi
hiyo Catherine Samba Panza amelazimika kukatiza safari yake ya kuelekea kwenye
Mkutano mkuu wa umoja wa mataifa.
Uchaguzi wa urais
umepangwa kufanyika mwezi Oktoba, mwezi mmoja kabla Baba Mtakatifu Francis
kutembelea Bangui.
CHANZO BBC SWAHILI
0 maoni:
Post a Comment