Utawala nchini Austria
unasema kuwa utatoa treni zaidi hii leo kusafarisha wahamiaji kutoka nchini
Hungary ambapo wengi walikwama kwa siku kadha.
Takriban watu 10,000
wanaaminika kuingia nchini Austria siku ya Jumamosi wengine wakisafiri moja kwa
moja kwenda nchini Ujerumani.
Umati wa watu
ulikusanyika mjini Munich hiyo jana kuwashangilia wahamiaji hao walipowasili.
Ujerumani inasema kuwa
kwa kulegeza kwa muda sheria za uhamiaji za muungano wa ulaya, imesaidia kuzuia
janga la kibinadamu kati ya mpaka wa Hungary na Austria.
CHANZO BBC Swahil.
0 maoni:
Post a Comment