Chama cha Wananchi
kimesema hakitashiriki maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi visiwani Zanzibar
kutokana na utata kuhusu matokeo ya uchaguzi.
Chama hicho kupitia
taarifa kimesema maadhimisho hayo yatafanyika “Serikali ikiwa inaongozwa na
viongozi ambao hawana uhalali na ridhaa ya wananchi”.
“CUF tumesisitiza mara zote kwamba hatukubaliani na uamuzi (wa kufuta matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar),” inasema taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Mshauri wa Katibu Mkuu wa CUF Mansoor Yussuf Himid.
“Tunapenda kutumia
fursa hii kuwaeleza wananchi wa Zanzibar kwamba viongozi wetu hawatoshiriki
katika shughuli walizopangiwa katika ratiba ya sherehe hizi.”
Siku ya Mapinduzi
huadhimishwa kila mwaka tarehe 12 Januari kukumbuka tarehe 12 Januari, 1964,
siku ambayo Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ilitangazwa na Rais wa kwanza wa
Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
CHANZO bbcswahili
0 maoni:
Post a Comment