Rais wa Rwanda Paul
Kagame ametangaza kwamba atawania urais kwa muhula wa tatu baada ya muhula wake
wa sasa kumalizika 2017.
Kiongozi huyo alitoa
tangazo hilo kwenye ujumbe wake wa mwaka mpya mnamo Ijumaa.
"Mumeniomba
niongoze nchi hadi baada ya 2017. Kwa kuzingatia umuhimu wa hili kwenu, sina
budi ila kukubali,” alisema Bw Kahame kwenye ujumbe wake uliopeperushwa moja
kwa moja kupitia runinga.
Hata hivyo aliongeza
kwamba hakusudii kuongoza Rwanda hadi kufa kwake.
0 maoni:
Post a Comment