Rais wa Urusi Vladimir
Putin ametia saini karatasi mpya ya sera ya kitaifa kuhusu usalama ambayo
inataja mpango wa upanuzi wa shirika la kujihami la Nato kama hatari kwa
usalama.
Stakabadhi hiyo inasema
“sera huru ya nyumbani na kigeni” ya Urusi imeifanya Marekani na washirika wake
kuchukua hatua.
Inayatuhumu mataifa
hayo kwa kujaribu kudhibiti masuala muhimu duniani.
Mzozo nchini Ukraine,
ulioanza 2014, umeathiri sana uhusiano kati ya Urusi na nchi za Magharibi.
Waraka huo kwa jina
Mkakati wa Usalama wa Kitaifa ulitiwa saini na Rais Putin Alhamisi, na ni wa
karibuni zaidi katika msururu wa stakabadhi za serikali zinazokosoa shirika la
kujihami la nchi za Magharibi la Nato.
Mwaka 2014, Urusi
ilitangaza kwamba ingebadilisha sera yake ya kijeshi kuzingatia mzozo wa
Ukraine na kuwepo kwa Nato mashariki mwa Ulaya.
kutoka BBCSwahili
0 maoni:
Post a Comment