MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

SUMATRA, YATANGAZA NAULI ZA MA-BUS MWENDO KASI, NI 400/=, 650/= NA 800. KUJUA ZAIDI SOMA KUPITIA LINK YETU.

DART-7
Wakati usafiri wa mabasi ya mwendo kasi ukitajia kuanza safari zake wiki hii, Hatimaye Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) yatangaza nauli zitakazo tumika kwa mabasi yaendayo kasi kuwa ni 400, 650 na 800 kwa safari za Mbezi mwisho hadi Kivukoni.

Akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Giliard Ngewe amesema nauli kutoka Mbezi mwisho hadi Kimara Sh400, na nauli ya Sh650 itatumika maeneo ya Kimara kwenda Kivukoni, Kimara –Kariakoo, Kimara – Morocco, Kariakoo – Kivukoni.

Amesema nauli ya Sh800 Mbezi Mwisho-Kimara –Kivukoni, kivukoni-Kimara- Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho-Kimara- Kariakoo, Kariakoo-Kimara-Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho Kimara- Morocco,na Morocco- Kimara-Mbezi Mwisho.

“Chombo chochote cha usafiri hakitaruhusiwa kutumia barabara za mwendo kasi kuanzia kesho, watakao kiuka agizo watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufutiwa reseni za biashara zao” amesema.

Source:Mwananchi

Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment