MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

UN YAISIHI KENYA KUTOFUNGA KAMBI ZA WAKIMBIZI


Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia wakimbizi UNHCR limeitaka serikali ya Kenya kubatilisha msimamo wake wa kutaka kuzifunga kambi mbili za wakimbizi za Dadaab na Kakuma nchini humo.

Serikali ilisema Ijumaa iliopita kwamba kambi hizo mbili zitafungwa kufuatia wasiwasi wa usalama na ukosefu wa fedha.

Ilitoa tangazo kama hilo awali,lakini wakati huu serikali imesema kuwa inazifunga idare zake za wakimbizi katika kile kinachoonekana kama hatua ya kwanza ya kusitisha uhifadhi wa wakimbizi 600,000.

Wengi wao ni raia wa Somalia na Sudan Kusini.

''Tumelipokea na wasiwasi mkubwa tangazo hilo'',lilisema shirika hilo katika taarifa yake.Iliongezea:
La kushangaza ni kwamba hali ilivyo Somalia na Sudan Kusini inayowafanya raia kutoroka haijatatuliwa

Chanzo BBC Swahili

Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment