Ndoa za wapenzi wa jinsia moja zimetawala kampeni katika siku za mwisho za kampeni nchini Australia.
Chama tawala cha kihafidhina kimeahidi kupigia kura swala hilo iwapo kitarudi katika mamlaka katika uchaguzi wa wikendi hii.
Lakini swali ni,je chama hicho kitaunga mkono matokeo ya kura hiyo iwapo yataunga mkono ndoa hizo.
Wakati huohuo kanda ya video imejitokeza kuhusu kiongozi wa upinzani Bill Shorten anayeunga mkono mpango wa kulipigia kura swala hilo.
Wiki iliopita bw. Shorten aliushtumu mpango wa serikali akiutaja kuwa wa kibaguzi na kupendekeza kura ya bunge kuamua kuhusu swala hilo.
Lakini aliliambia kundi moja la dini ya kikristo mwaka 2013 kwamba angeuruhusu uma kulipigia kura swala hilo badala ya kuliwachia wabunge.
0 maoni:
Post a Comment