MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Mourinho amkejeli tena Arsene Wenger

Mkufunzi Jose Mourinho amesema kuwa yuko tayari kuchukua jukumu la kuifunza Manchester United, lakini akaonekana pia kumkejeli meneja wa Arsenal Arsene Wenger.
Amesema ''niko mahala nitakapo''.
Raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 aliongezea: ''Nadhani ni kazi ambayo kila mtu anahitaji na sio wengi ambao huipata na mimi nimeipata''.
Alipoulizwa iwapo ana chochote cha kujionyesha baada ya kufutwa kazi akiwa Chelsea, alijibu, akionekana kumrejelea Wenger: ''Kuna mameneja ambao hawajashinda mataji kwa kipindi cha miaka 10 iliopita. Wengine bado kabisa. Mara yangu ya mwisho kushinda taji ni mwaka uliopita''.
Mkufunzi huyo wa zamani wa Chelsea anachukua mahala pake Louis Van Gaal,ambaye alifutwa kazi baada ya United kushinda kombe la FA mnamo mwezi Mei.
Mourinho anasema kuwa anachukizwa kuona kwamba United haitashiriki katika mechi za kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu ujao lakini akasisiiza kuwa yuko Old Trafford kushinda mataji.
Nataka kila kitu,alisema.Nataka kushinda mechi,nataka kucheza vizuri sitaki kufungwa magoli.nataka mashabiki kutuunga mkono.
''Ni kweli hatuwezi kupata kila kitu, lakini tunataka''
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment