MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Museveni aketi barabarani kupokea simu


Je ushwahi kupokea simu ya dharura ?
Je wewe hujitenga vipi na watu waliokaribu nawe ima ni mkeo ama hata wafanyakazi wenza iliupokee simu ya kibinafsi?
Na je katika enzi hizi za simu za kisasa au Smartphone wangapi wetu wanatumia simu za kale zisizo na touchscreen ?
Haya basi ,

Hayo sio maswali ya kipima joto,,,la!
Rais wa Uganda bwana Yoweri Kaguta Museveni alizua kihoja katika kijiji kimoja karibu na mpaka wa Uganda na Tanzania aliposimamisha msafara wake wa magari iliapokee simu faraghani.
Amini usiamini Rais Yoweri Museveni, alishuka kutoka kwenye gari lake rasmi akachukua kiti chake na kukiweka kando kando ya barabara mpya ya Isingiro ikipitia kijiji hicho cha Kyeirumba hadi Tanzania na kupokea simu faraghani.

Mzee Museveni kama vile baba wa taifa alitumia muda wake kufanya shughuli hiyo huku akiwapungia mkoo wapita njia.
Baada ya dakika 30 hivi raia wa kijiji hicho walishangaa kuwa miongoni mwa maafisa wakuu serikalini.

Ilikuwa ajabu sana kwao kumuoana Museveni akiwa ameketi barabarani.
Waganda katika mitandao ya kijamii wamesambaza picha hiyo ya rais museveni akizungumza kwa simu ambayo inaonekana kuwa sio ya kisasa.

Wengine wanamkejeli kwa kuhofia kudukuliwa huku wengine wakimgoa kwa kuketi barabrani
''kwani hangeweza kupokea simu yake ndani ya gari lake ?
''ni siri gani hiyo ambayo hakutaka hata walinzi wake wasikie,
''Ama ilikuwa ni #Besigyexit ? wakizungumzia kuachiliwa kwa dhamana kwa kiongozi wa upinzani Kizza Besigye.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment