Vikosi vya uokoaji vya majini vya
Italy vimesema vimeratibu uokoaji wa wahamiaji elfu sita na mia tano
katika bahari ya Mediterania siku ya jumatatu. Kwa mujibu wa vikosi
hivyo, hii ni oparesheni kubwa zaidi kuwahi kutokea katika miaka ya hivi
karibuni.
Taarifa za oparesheni hiyo ambayo ilihusisha vikosi
kutoka nchi mbalimbali zilitolewa katika mtandao wa Twitter, na
imeelezwa kuwa ni moja kati ya oparesheni kubwa ya uokoaji kuwahi
kutokea kwa miaka mingi. Katika moja ya oparesheni hizo, raia kutoka Eritrea na Somalia wameonekana wakiruka baharini huku wakikimbilia vikosi vya uokoaji.
Maelfu ya raia wa kiafrika, wengi wao wakitafuta maisha bora barani ulaya, mara nyingi husafirishwa katika madau ambayo hayana hadhi ya kuhimili mikiki mikiki ya bahari.
0 maoni:
Post a Comment