
Meneja wa klabu ya Celtic ya
Scotland Brendan Rogers amesema mchezaji wa klabu ya Barcelona ya
Uhispania ndiye mshambuliaji bora zaidi duniani.
"Kwa sasa, Luis ndiye mshambuliaji bora zaidi duniani. Na sidhani kuna swali au shaka kuhusu hilo. Kwanza, ukimzungumzia Suarez ni lazima umzungumzie yeye binafsi. Ni mmoja wa wachezaji watanashati zaidi.
Mnyenyekevu. Ana bidii sana. Ni mtu wa familia, ambaye hujitolea kwa hali na mali kwa soka na familia.
"Najivunia kufanya kazi naye kama binadamu kwa miaka miwili, na nilifurahia. Kama mchezaji soka, ndiye bora zaidi."
"Alijiunga na klabu bora zaidi duniani na akawaboresha. Barca haiwezi kuwa ilivyo sasa bila Suarez. Huwa twawasiliana."
Suarez alichezea Liverpool Rogers alipokuwa meneja.
Alihama klabu hiyo mwaka 2014. Mwezi Mei mwaka huu, alimsifu mkufunzi huyo akisema alimsaidia kujiimarisha.
Barcelona walikutana na Celtic hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2004, 2008, 2012 na 2013.
0 maoni:
Post a Comment