KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), leo imefanya mkutano wake utakaokuwa na ajenda
mbili katika kikao hiko.
Akizungumza na waandishi wa habari
Dar es Salaam jana, Afisa Habari wa TFF Bonifasi Wambura, alisema kutakuwa na
ajenda mbili katika kikao hiko ambalo moja ni kuhusu mkutano mkuu wa uchaguzi
wa TFF.
“katika kikao hiko cha kesho (leo),
ajenda kuu ni kuhusu swala la mabadiliko ya katiba mpya ya TFF, ambapo kamati
itapitia walaka zilizotolewa kwa vyama wanachama wa TFF kwa ajili ya kupiga
kura mchakato huo.
Na pia ajenda nyingine katika kikao
hiko itakuwa ikihusiana na mkutano wa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa TFF,”
alisema Wambura.
Wakati huo huo Wambura, aliupongeza
uongozi mpya wa Chama cha Soka Mkopa wa Dar es Salaam (DRFA), baada ya kushinda
katika uchgaguzi wake mkuu uliofanyika Juma tano.
0 maoni:
Post a Comment