Polisi nchini Kenya
inaendelea na msako wa kuutia mbaroni mtandao wa kundi la wapiganaji
linalojiita Islamic State ambalo linataka kukita mizizi yake nchini Kenya kwa
lengo la kufanya mashambulizi ya kigaidi dhidi ya wananchi wasio kuwa na hatia.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na inspekta mkuu wa polisi.
Kauli hiyo imetolewa
baada ya polisi nchini Kenya kuwatia mbaroni watu wawili wanaoshukiwa kuwa ni
wafuasi wa kundi la wapiganaji la IS.
Kwa mujibu wa polisi,
kukamatwa kwa wawili hao ambao ni Mwangolo Mgutu na Abubakar Jillo Mohammed
kumezuia mashambulizi ya kigaidi yaliyokuwa yakipangwa kwa kutumia vilipuzi na
silaha nyingine katika mji wa Nairobi na Mombasa.
Mbali na kukamatwa kwa
washukiwa hao wawili, polisi pia imepata vitu mbalimbali katika nyumba ya
Kiguzo Mwangolo kama vile misumari, betri, waya na mbolea ambazo inadaiwa
zingetumika kutungezea bomu la nyumbani.
Polisi imeendelea
kusema, katika uchunguzi wake wa mwanzo, imebaini kuwa Kiguzo na Abubakar ni
miongoni mwa waandishi wa makala iliyokuwa inasambaa kupitia mtandao ambao
ilikuwa ikielezea kuwepo kwa kundi la Jahba katika eneo la Afrika Mashariki
ambalo limetangaza kumuunga mkono kiongozi wa ISIS Abubakr Al-Baghdadi.
Kutoka BBC Swahili.
0 maoni:
Post a Comment