Kikosi cha watoto wa Jangwani Yanga Afrika,
wamefikia mwisho katika majadiliano na Hamisi Kiiza, baada ya pande mbili hizo
kukubaliana kuongeza mkataba mpya na mshambuliaji huyo.
Kiiza , anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili
na kikosi hicho cha mabingwa wa ligi Kuu ya Tanzania Bara, haya ni maneno yake “"Tumefikiana
na klabu yangu - sasa nitaongeza mkataba na kuendelea kuitumikia klabu ya Yanga
msimu ujao. Baada ya kumaliza taratibu zote za kusaini mkataba mpya nitarudi
nyumbani Uganda mara moja kabla ya kurudi kuja kujiunga rasmi na wenzangu kwenye
pre-season," Kiiza alisema.
0 maoni:
Post a Comment