Maafisa wa uchaguzi
waliokuwa wametekwa nyara Kaskazini mwa Mali wiki moja kabla ya uchaguzi mkuu
wa urais wameachiliwa huru.
Maafisa wanasema kuwa
wafanyakazi hao walikamatwa Jumamosi katika eneo laTessalit wakati wakitoa kadi
za kupigia.
Waasi wa Tuareg
wanashukiwa kuwa wao ndio waliowakamata maafisa hao.
Hivi maajuzi Mali
iliondoa sheria ya hali ya hatari iliyokuwa imewekwa tangu Januari wakati
ambapo Ufaransa ilipoingili kati mgogoro wa kisiasa uliokuwa unakumba taifa
hilo na kukabiliana na waasi waliokuwa wameteka Kaskazini mwa nchi.
Gavana wa jimbo la
Kidal Kaskazini, Adama Kamissoko, aliambia shirika la habari la Associated
Press kuwa wafanyakazi hao walikuwa wametekwa nyara na wapiganaji wa Tuareg.
Waliachiliwa huru
Jumapili na kuchukuliwa na wanajeshi wa Ufaransa waliowapeleka katika kambi ya
Jeshi ambayo haiko mbali sana na eneo la Tessalit.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment