Rais Jakaya Kikwete, amewaongoza watanzania katika kutoa heshima zao za mwisho kwa wanajeshi saba wa Tanzania, walipoteza maisha katika mapigano nchini Sudan.
Wanajeshi hao walikuwa nchini humo kwa kulinda amani
katika eneo la Darfur, nchini Sudan, mnamo tarehe 13 mwenzi julai.
Miili ya wanajeshi hao iliwasili nchini Tanzania
siku ya jumamosi jijini Dar es salaam, na kupokewa na watanzania wenye upendo,
ambao walikuwa katika udhuni mkubwa, ambao waliongozwa na Makamu wa Rais
DK-Gharib Bilal, katika uwanja wa ndege wa Mwl- Julius Nyerere.
Wanajeshi hao
wanaagwa katika makao makuu ya jeshi jijini Dar es salaam , maeneo ya Upanga,
pia Rais Kikwete ndiye anayeongoza Salam za Heshima mbele ya Ndugu na Jamaa wa
wanajeshi hao sambamba na watanzania wote
0 maoni:
Post a Comment