Wafuasi
wa rais wa Misri aliyeondolewa madarakani na jeshi,Mohamed Morsi wamesema zaidi
ya watu laki moja na ishirini wameuwawa katika mapambano na vikosi vya ulinzi
na usalama mjini Cairo.
Polisi waliingia katika mkusanyiko
wa usiku wa wafuasi wa Morsi saa chache baada ya waziri wa mambo ya ndani
kusema wafausi wa Morsi na chama chao cha Muslim Brotherhood waliokusanyika
kwenye viunga vya msikitini wa Rabba Al Adawiya lazima waondoke.
Muslim Brotherhood wamelilaumu jeshi
kwa kuwapiga risasi na kuwauwa wafuasi wao.
Daktari katika hospitali ya muda
amesema watu wawili walifikishwa wakiwa kichwa na viwili wili vyao
vimetenganishwa huku wengine wakiwa na matundu ya risasi vichwani na kifuani.
Hospitali hiyo imekuwa katika hali
ngumu ya kumudu miili ya marehemu na majeruhi wanaofikishwa hospitalini hapo.
Mwandishi wa BBC anasema ni mapigano
mabaya zaidi tangu jeshi limuondoe rais Morsi madarakani.
Wakati huo huo, Uingereza imekemea
matumizi ya nguvu yanayopoteza maisha ya watu nchini Misri.
Waziri wa masuala ya kigeni William
Hague amewataka wenye mamlaka kumaliza mapigano na vurugu hizo.
Amesema wale waliohusika na mauaji
hayo ni lazima wawajibike na haki ya wanaoandamana kwa amani ni wajibu ilindwe.
Bwana Hague pia amelitaka jeshi
kuwachilia huru viongozi wa Muslim Brotherhood waliowekwa kizuizini akiwemo
rais Mohamed Morsi.
0 maoni:
Post a Comment