Wafuasi
wa rais wa Misri aliyeondolewa madarakani na jeshi,Mohammed Morsi wameendelea
kupiga kambi katika msikiti wa Rabaa al-Adawiya mashariki mwa mji mkuu wa
Cairo,
Ikiwa ni siku moja tu baada ya
ghasia kali kuzuka.
Waandamanaji hao wameweka vizuizi
katika kambi yao na kuapa kutoondoka licha ya mapambano kati yao na vikosi vya
ulinzi na usalama.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani
John Kerry amesitikitishwa na ghasia zinazoendelea nchini Misri.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari,bwana Kerry amesema kuwa wakati huu ni muhimu sana kwa taifa hilo na
akatoa wito kwa serikali hiyo kuheshimu haki ya raia kuandamana kwa amani na
uhuru wa kujieleza.
Mwandishi wa BBC anasema hali sasa
imetulia kiasi licha ya vurugu kutokea katika viunga vingine vya mji wa Cairo.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment