Chama cha waziri mkuu wa nchini Zimbabwe, kinadai
kuwa mmoja wa offisa mkuu wa chama hicho amekamatwa baada ya kuwakilisha
ushaidi wa udanganyifu mbele ya tume ya uchaguzi nchini humo.
Morgen Komichi aliifahamisha mamlaka baada ya
kugundua makaratasi ya kupiga kura yalikuwa yamewekwa katika kituo cha kupiga
kura mjini Harare ambapo maafisa wa jeshi walipiga kura za mapema katika
uchaguzi huo.Alisema masanduku yote ya kura yaliyokuwa na kura za chama cha Movement For Democratic Change (MDC) yalitupwa.
MDC kinachoongozwa na waziri Mkuu Morgan Tsvangirai, kimekuwa katika serikali ya umoja wa kitaifa na rais Robert Mugabe wa ZANU PF , Umoja ambao umekuwa na mashaka ndani yake.
Uchaguzi nchini Zimbabwe umefanyika mapema Jumatano iliyopita.
Chanzo cha Habari hii ni BBC
0 maoni:
Post a Comment