NICK MINAJ-Ametokezea kwenye jarida la Marie Claire,
katika toleo la mwaka huu, kutokana na Picha yake kuwekwa kwenye kurasa ya
mbele ya Magazine, hiyo inamfanya kuwa msanii wa kwanza kutokezea mwaka huu.
Pia msanii huyo alifunguka na kusema kuwa anapenda
siku moja kuwa mama, hivyo anajiandaa kuwa kwa jambo hilo, aliendelea kuongea
na kutoa ushauri kwa wanawake wenzake kwa kusema kuwa “ wanawake wanatakiwa
wasiangaike na wanaume na badala yake kuzingatia elimu, na kujituma kwa sababu
wanaume wengi wanawapenda wanawake wanaojituma” hayo aliyasema Minaj.
Kuuhusu Muziki alifunguka na kusema kuwa anataka
kuachia Albam Tatu kabla ya kuachana na muziki.
0 maoni:
Post a Comment