Waziri wa mambo ya nje
wa Marekani John Kerry, amesema kuwa jeshi la Misri, lilikuwa linarejesha
demokrasia nchini humowakati lilipomwondoa mamlakani aliyekuwa rais Mohammed
Morsi mwezi jana.
Bwana Kerry alisema
kuwa kuondolewa kwa Morsi, ilitokana na mambo ya mamilioni ya watu wa Misri .
Matamshi ya Kerry
yanakuja huku polisi wakijiandaa kuwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa
Morsi waliopiga kambi mjini Cairo.
Waziri wa mambo ya
ndani wa Misri, ameahidi kuwa wafuasi wa Morsi, kuwa nguvu kaitatumika
kubailiana nao ikiwa wataondoka kutoka eneo hilo kwa hiari.
Baraza la mawaziri la
Misri liliamuru jeshi kumaliza maandamano hayo ambayo limeitaja kuwa tisho la
usalama kwa nchi.
Licha ya kuombwa
kuingilia mgogoro wa kisiasa Misri, Marekani imekataa kutaja hatua ya kumwondoa
mamlakani Morsi kama mapinduzi ya kijeshi.
Kwa kufanya hivyo
serikali ya Marekani itahitajika kusitisha msaada wake kwa taifa hilo wa dola
bilioni moja nukta tano ambao hutolewa kila mwaka.
John Kerry ametoa
kauli yake wakati wa mahojiano kwenye televisheini moja nchini Pakistan.
Wadadisi wanasema kuwa
matamshi ya Kerry pia yatatafsiriwa kama uungwaji mkono wa serikali ya muda ya
Misri.
Chanzo cha Habari hii ni BBC
0 maoni:
Post a Comment