Mjumbe mmoja wa Marekani
anatarajiwa kuwasili Korea Kazkazini hii leo katika ziara inayolenga kuirai
serikali ya taifa hilo kumwachilia Kenneth Bae, aliyekamatwa nchini humo mwezi
Novemba, mwaka uliopita.
Katika ziara ya kwanza iliofanywa na
afisa wa ngazi ya juu kutoka Marekani katika kipindi cha miaka miwili, balozi
Robert King anatarajiwa kuomba kuwachiliwa kwa Bae kwa misingi ya kibinaadamu.
Raia huyo wa Marekani ambaye ni kiongozi
wa dini alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela na kazi ngumu kwa kile Korea
Kazkazini inadai ni uvamizi.
Bwana Bae alilazwa hospitalini mapema
mwezi huu baada ya uzani wake kupungua kwa ghafla.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment