Msanii wa muziki wa Dance nchini Tanzania, Mzee
Muhidin Ngurumo, aliyekuwa katika Bend ya Msongo Ngoma, ameamua kustahafu
muziki, mara baada ya kuutumikia kwa miaka 53, iliyopita.
Mwanamuziki huyo alisema kuwa ameamua kuachana na
muziki kutokana na sababu mbili kuu ambazo ni kutokana na umri wake kuwa
mkubwa sana (73) pia anataka kuwaachia vijana nafasi , sambamba na kumpa nafasi
mke wake kutokana na muda wote mkewe kutokuwa na nafasi ya kutosha kwake, kila
sikumalikuwa anarudi usiku wa manane akitokea kazini.
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 73, alisema umri
wake ni mkubwa sana hivyo hawezi tena kwenda na kasi ya muziki kwa sasa. Alisistiza
kuwa bado ataendelea kutoa ushauri kwa vijana katika swala la muziki.
0 maoni:
Post a Comment