Rais mteule wa Iran Hassan Rouhani anaapishwa katika sherehe mjini Tehran
ambapo atapewa idhini ya kiongozi wa kidini nchini humo, Ayatollah Ali
Khamenei.
Rouhani ambaye alikuwa
mpatanishi kwenye mazungumzo ya mradi wa nuklia wa Iran, alishinda uchaguzi wa
urais nchini Iran katika duru ya kwanza.
Wakati wa kampeni zake
rais huyo mteule aliahidi kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, na alisema
ataimarisha uhusiano kati ya taifa hilo na jamii ya kimataifa ambao uliharibika
zaidi wakati wa utawala wa Rais Mahmoud Ahmedinejad.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment