Maelfu ya watoto wanaofanya
kazi katika machimbo ya madini nchini Tanzania wanakabiliwa na tishio kubwa la
kupata magonjwa na hatimaye kufa.
Shirika la kutetea haki za kibinadam la
Human Rights Watch, limefichua ushahidi zaidi kuhusu unyanyazaji wa watoto
nchini Tanzania, baadhi yao wenye umri wa miaka minane ambao wanafanya kazi kwa
zamu, katika migodi ya madini iliyoko chini ya ardhi, kwa saa ishirini na nne.
Shirika hilo limesema watoto hao
wanakabiliwa na tishio la kuvuta hewa ya sumu inayotokana na uchimbaji wa
madini ya dhahabu na wakati mwingine kuuawa wakati migodi hiyo, inapoporomoka
nyingi zikiwa hazina leseni.
Tanzania ina sheria kali inayozuia
watoto kufanya kazi katika machimbo ya madini lakini shirika hilo limesema,
serikali ya rais Jakaya Kikwete ni sharti iimarishe juhudi zake za kuhakikisha
sheria hizo zimetekelezwa.
Kutoka BBC.
0 maoni:
Post a Comment