Wapiganaji wa Boko
Haram wamewaua watu 87 katika shambulio katika Jimbo la Borno nchini Nigeria.
Mashahidi wanasema
kuwa wapiganaji hao waliteketeza nyumba kadhaa katika tukio hilo la kutisha
mnamo Jumanne usiku.
Shambulio hili
limetokea siku chache baada ya makabiliano makali kati ya jeshi na wapiganaji
wa Boko Haram
Wanamgambo hao
waliokuwa wamevelia magwanda ya jeshi, waliweka vizuizi barabarani nje ya mji
wa Benisheik na kuwapiga risasi wale waliokuwa wanajaribu kutoroka.
Kwa mujibu wa taarifa
za mashahidi , wapiganaji hao waliteketeza nyumba katika shambulizi hilo la
Jumanne.
Kundi la Boko Haram,
ambalo linapigania linachosema ni taifa la kiisilamu nchini Nigeria, limekuwa
likifanya mashambulizi sawa na haya kuanzia mwaka 2009.
Jeshi linadai kuwa
Agosti mwaka huu, kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau na naibu wake Momodu
Bama waliuawa , ingawa hakuna taarifa za kujitegemea kuthibitisha hilo.
Mawasiliano katika
jimbo la Borno, yamekumbwa na hitilafu, tangu mwezi Mei, wakati hali ya hatari,
ilipotangazwa katika jimbo hilo na majimbo mengine mawili.
Lakini mashambulizi
yameongezeka sana hivi karibuni tangu jeshi kuanza kukabiliana na kundi hilo
katika maeneo yaliyoathirika zaidi.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment