Viongozi wa Afrika
wanatarajiwa kukutana mwezi ujao mjini Addis Ababa Ethiopia, kujadili msimamo
wa bara hili kuhusu iwapo watajiunga na Kenya katika kujiondoa kutoka Mahakama
ya Kimataifa ya Uhalifiu - ICC.
Mkutano huo unafuatia
ombi la Kenya kutaka kikao cha dharura cha Umoja wa Afrika kujadili kesi
zinazowakabili Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.
Mwandishi wa BBC mjini
Addis Aabab, Emmanuel Igunza anasema kuna dalili kuwa ombi hilo la Kenya
limeanza kuungwa mkono na mataifa mengi barani.
Kwa sasa hakuna dalili
kuwa kuna msimamo mmoja kuhusu ikiwa wanachama 54 wa Muungano wa Afrika
waliotia saini mkataba wa Roma wanataka kujiondoa, lakini marais wa nchi hizo
bado watajadili uwezekano wa wanachama 34 wa mkataba wa Roma uliounda mahakama
ya ICC watajiondoa ICC.
Tangu kuanza kwa kesi
ya Naibu rais wa Kenya William Ruto katika mahakama ya ICC wiki jana, na ile ya
Rais Kenyatta ikitarajiwa kuanza mwezi Novemba, dalili zimeonekana kuwa wengi
hawana imani na mahakama hiyo wakiiona kama chombo cha nchi za Magharibi
kukandamiza waafrika.
Kikao cha dharura sasa
kimepangwa kujadili swala hilo baada ya Kenya kuonekana kutaka kuungwa mkono
katika azma yake ya kujiondoa ICC.
Kuna uwezekano wa nchi
wanacahama wa mkataba wa Roma kujiondoa ICC lakini bado kuna nafasi ya maombi
mengine kufanywa kuhusiana na hilo.
Kutoka BBC,
0 maoni:
Post a Comment