Marekani inaonesha kuwa iko tayari kuacha kutaja hatua ya
kijeshi katika azimio lolote la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu
Syria.
Maafisa wa ikulu ya Marekani walisema
kumepatikana maendeleo katika juhudi za kupata azimio linalokubalika, ambalo
linaweza kujadiliwa baada ya ujumbe wa wakaguzi wa silaha za kemikali wa Umoja
wa Mataifa kutoa ripoti yao Jumatatu.
Mazungumzo baina ya Marekani na Urusi
kuhusu namna ya kudhibiti shehena ya silaha za kemikali za Syria yanaendelea
kwa siku ya tatu.
Huku nyuma, Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ban ki-Moon, anasema anataraji kutafanywa duru ya pili ya mazungumzo
ya amani kuhusu Syria, mwezi ujao.
Akizungumza kwenye televisheni ya
Ufaransa, Bwana Ban alisema amezungumza na mjumbe wa Jumuia ya Nchi za Kiarabu,
Lakhdar Brahimi kuhusu swala hilo hapo Ijumaa na wote wawili wanaona hilo ni
jambo muhimu.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment