Baadhi ya wabunge wa upinzani nchini Kenya wameondoka bungeni wakati
mjadala mkali ukiendelea kuhusu kuunga mkono au kupinga nchi hiyo kujiondoa
kutoka katika mahakama ya kimataifa ya ICC.
Wabunge hao wameondoka bungeni baada ya
kusema kuwa kamwe hawataungana na upande wa serikali kuunga mkono hoja hii ya
kujiondoa kutoka katika mahakama ya ICC.Ni kutokana na kuwa kwamba upinzani una
idadi ndogo zaidi ya wabunge bungeniWabunge nchini Kenya wanatarajiwa kukutana kwa dharura hii leo kujadili ikiwa nchi hiyo itajiondoa kwenye mahakama ya kimataifa ya ICC au la.
Hatua hii ya wabunge
inakuja zaidi ya wiki moja kabla ya kuanza kwa kesi dhidi ya naibu Rais wa
Kenya Williiam Ruto kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2008.
Ruto anakabiliwa na
mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Rais Uhuru Kenyatta
pia anatarajiwa kufika katika mahakama hiyo mwezi Novemba kwa kesi dhidi yake.
Wawili hao
wanashtakiwa kwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mwishoni mwa mwaka
2007.
Msemaji wa ICC
ameambia BBC kuwa kesi hiyo itaendelea hata ikiwa Kenya itajiondoa kwenye
mkataba wa Roma uliopelekea kuanzishwa kwa mahakama hiyo.
Bwana Fadi El
Abdallah, alisema kuwa itachukua karibu mwaka mmoja kwa mchakato wa nchi yoyote
yoyote ile kujiondoa kutoka katika mahakama ya ICC na hii bila shaka inaathiri
tu kesi zilizokuwa mbele ya mahakama hiyo kwa wakati huo.
Hii ni hatua ya
dharura inayochukua serikali kujitoa katika Mkataba wa Roma wa mahakama hiyo
ulioidhinishwa na Umoja wa mataifa mnamo tarehe 17 July, mwaka1998.
Kenya inataka kutoa
mfano wa kuwa nchi ya kwanza Afrika kuchukua hatua hiyo licha ya kwamba uamuzi
huu hautoathiri kwa namna yoyote kesi zinazoendelea sasa katika mahakama ya
ICC.
Mahakama hiyo ya kimataifa
imesema kwamba kesi hizo zitaendelea hata iwapo Kenya itajitoa.
Imesema itaichukua
Kenya kiasi ya mwaka mmoja kabla ya kukubaliwa ombi hilo la kutaka kujiondoa
katika mkataba wa Roma na hilo litaathiri tu kesi zitakazozuka baada ya muda
huo.
Haya yanajiri wakati
makamu wa rais William Ruto anatarajiwa kuondoka Kenya kueleka Hague Uholanzi
wiki ijayo kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadaamu katika mahakama
hiyo ya ICC, kesi inayoanza tarehe 10 mwezi huu.
Wote wameshtakiwa kwa
kuhusika katika ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.Kesi
dhidi ya rais Uhuru Kenyatta inatarajiwa kuanza tarehe 12 mwezi Novemba.
Kutoka BBC.
0 maoni:
Post a Comment